Toleo la:

6/10/2021

Kila mtu mwenye umri wa miaka 12 na zaidi Oregon anaweza kupata chanjo ya COVID-19. (Watoto wenye umri wa miaka 12-17 wanaweza kupata chanjo ya Pfizer tu)

Hata ikiwa umepata chanjo, endelea kulinda afya yako na afya ya familia na marafiki zako: nawa mikono yako, dumisha umbali wa futi 6 kati yako na wengine, na punguza mikusanyiko. Vaa barakoa yako kwenye halaiki ya watu.

Chanjo za COVID-19 zitasaidia kuilinda jamii dhidi ya COVID

Ninawezaje kupata chanjo ya COVID-19?

Tafuta eneo la kupata chanjo kwa kutumia Kionyeshi cha Chanjo cha Oregon. Maeneo mengi hutoa huduma za usafiri na kuratibu miadi. Kliniki zijazo za Chanjo ya COVID-19 katika Multnomah County.

 • SI lazima uwe raia wa Marekani. 

 • Kupata chanjo HAKUTAATHIRI hali yako ya uhamiaji au kuhesabika kama mgeni aliyepata msaada wa serikali. 

 • Huna haja ya kuwa au kutoa namba yako ya hifadhi ya jamii. 

 • Huna haja ya kuwa na kitambulisho. 

 • Huna haja ya kuwa na bima ya afya.

 • Chanjo ni bure.

Chanjo kwa watoto wa miaka 12 na zaidi

 • Watoto wa miaka 15-17 hawana haja ya kuwa na mtu mzima, na hawahitaji idhini ya mzazi katika jimbo la Oregon. Tunawahimiza vijana kuwahusisha watu wazima wanaoaminika katika kufanya uamuzi wa kimatibabu. 

 • Watoto wenye umri wa miaka 12-14 lazima waandamane na mzazi, mlezi au mtu aliyeteuliwa na mzazi/mlezi.

 • Ikiwa mtu mwingine asiye mzazi au mlezi yuko na umri wa miaka 12-14, atahitaji kutoa uthibitisho wa idhini ya mzazi/mlezi. Mzazi au mlezi pia anapaswa kupatikana kwenye simu kujibu maswali kadhaa ya matibabu. Uthibitisho wa idhini ni wa ama:

  • Fomu ya idhini iliyosainiwa, au

  • Ujumbe ulioandikwa au kuchapishwa ambao unajumuisha jina la mzazi/mlezi, uhusiano wao na mhusika, tarehe ya kuzaliwa kwa mhusika, taarifa inayosema mzazi/mlezi anakubali kijana huyo mdogo kupewa chanjo, na saini ya mzazi/mlezi.

Unaweza pia:

Nyenzo zaidi za Chanjo ya COVID-19

Vifunika uso

Tazama mwongozo wa Serikali wa vifunika uso

Vizuizi

Vizuizi vingi bado vipo kwenye Multnomah County. Kila County ya jimbo la Oregon imepewa Kiwango cha Hatari kulingana na jinsi COVID-19 inavyoenea katika jamii zetu. Taarifa mpya kuhusu viwango vya hatari zinatolewa kila baada ya wiki mbili. Pata kiwango cha hatari cha sasa cha Multnomah County kwenye Tovuti ya Virusi vya Korona ya Oregon. Angalia shughuli ambazo zinaruhusiwa kwenye Mwongozo wa sekta wa Jimbo kulingana na kiwango cha hatari cha county.

Zuia Kuenea kwa COVID-19 

Virusi ambavyo husababisha COVID-19 huambukiza kwa urahisi kutoka kwa mtu mmoja. Ili kuepuka kuugua:

 • Nawa mikono yako mara kwa mara kwa angalau kwa sekunde 20

 • Vaa barakoa unapotoka nje

 • Epuka kugusa uso wako

 • Funika unapokohoa na kupiga chafya

 • Kaa angalau futi 6 kutoka kwa watu ambao huishi nao

 • Punguza idadi ya watu katika mikusanyiko, iwe mifupi, na ifanyiwe nje wakati wowote inapowezekana

 • Safisha na kuua vimelea kwenye maeneo yanayoguswa sana

 • Punguza safari na ukae karibu na nyumbani

 • Pata chanjo

Watu wenye matatizo ya kudumu ya afya, kama vile pumu, ugonjwa wa kisukari, au ugonjwa wa moyo au mapafu, wako katika hatari kubwa ya kuugua sana na COVID-19. Tazama vidokezo vya jinsi ya kuwa salama ikiwa unaishi na watu wengi.

Ikiwa unajisikia kuumwa

Ukianza kuhisi kuumwa - haswa na homa na kikohozi:

 • Kaa nyumbani na mbali na wengine. 

 • Piga simu kwa daktari wako au kliniki ili kuona kama unapaswa kupimwa.

 • Kaa nyumbani hadi daktari au kliniki yako itakapokushauri kuwa unaweza kuwa karibu na wengine tena.

 • Fanya vitu ambavyo kwa kawaida hufanya ili kujisikia vizuri: lala, pumzika, kunywa maji mengi.

 • COVID-19 haina tiba maalum.

Tafuta huduma ya dharura mara moja ikiwa wewe au mtu wa umri wowote anaonyesha ishara zozote za tahadhari za dharura:

 • Kupumua kwa shida

 • Maumivu yanayoendelea au shinikizo kwenye kifua

 • Kuanza kuchanganyikiwa

 • Kutokuwa na uwezo wa kuamka au kukaa macho

 • Midomo au uso wa hudhurungi

 • Maumivu makali ya tumbo

 • Piga simu 911 au piga simu kabla ya kutembelea kituo chako cha dharura cha eneo lako.

 • Mwambie opereta kwamba wewe au mtu anayehitaji msaada anaweza kuwa na COVID-19.

Tazama Njia 10 za Kudhibiti Dalili za Upumuaji Nyumbani kutunza afya yako.

Upimaji wa COVID-19

Unapaswa kupimwa ikiwa una dalili za COVID-19 au ikiwa ulitangamana kwa karibu na mtu aliye na COVID-19. Kutangamana kwa karibu kunamaanisha kuwa karibu na mtu ndani ya futi sita kwa dakika 15 au zaidi kwa muda wa siku, ukiwa na au bila barakoa.

Kupata huduma kwa ajili ya familia yako

Ikiwa huna daktari, piga simu 211 au Vituo vya Afya vya Msingi vya Multnomah County 503-988-5558. Huduma za ukalimani zinapatikana. Katika kliniki ya Multnomah County

 • Huna haja ya kuwa na bima ya afya.

 • Huna haja ya kuwa na mapato.

 • Unaweza kupata huduma ya afya bila ya kujali hali yako ya uhamiaji.

 • Hatutoi taarifa yako kwa maafisa wa usalama au maafisa wa uhamiaji.

Uhamiaji na Utekelezaji wa Forodha una sera ya kuzuia kukamatwa katika vituo vya huduma za afya, kama vile hospitali, ofisi za daktari, kliniki za afya, na vituo vya huduma za dharura. 

Ikiwa utapata matibabu au huduma za COVID-19, haitathiri maombi yako ya makazi ya kudumu Marekani. Soma zaidi kuhusu Msaada Serikali.

Nyenzo

Maswali?

Tembelea 211 info au piga simu 2-1-1 kati ya 2-8 asubuhi hadi 5-11 usiku Huduma za tafsiri zinapatikana.