Ilisasishwa tarehe 05 Aprili, 2022

Kwenye ukurasa huu:

Hatua ya kuchukua ukipokea notisi ya kufukuzwa nyumba

211info: Ikiwa wewe au wanafamilia wenzako mtapokea notisi ya kufukuzwa kwa kutolipa kodi, piga 2-1-1 haraka ili ufahamu zaidi kuhusu msaada wa haraka wa kodi unaoweza kukusaidia kuepuka kufukuzwa. Timu ya watetezi wa Kaunti wa watu wanaofukuzwa inaweza kutoa msaada wa haraka wa kifedha na kisheria ili kuwasaidia wapangaji katika Kaunti ya Multnomah kukaa nyumbani mwao. Piga simu hata kama tayari umetuma ombi la msaada kupitia tovuti ya mtandaoni ya jimbo au shirika la jamii.

Pakua hati hii ya maelezo kwenye Kituo cha Sheria cha Oregon ili upate maelezo zaidi kuhusu ulinzi dhidi ya kufukuzwa nyumba.

Mahali pa kupata usaidizi wa kisheria

Wapangaji wanaohitaji ushauri wa kisheria wanaweza kupata usaidizi kutoka kwa rasilimali za jumuiya kama vile Kituo cha Sheria cha Oregon, Muungano wa Jamii wa Wapangaji au Huduma za Msaada wa Kisheria Oregon.

Ustahiki kupokea msaada wa kodi katika Kaunti ya Multnomah

Happy black family hugging and embracing on couchKama wewe ni mkaazi wa Multnomah County na unasumbuka kulipa kodi yako (ya sasa au iliyopita) kwasababu ya janga, huenda utastahili kupokea usaidizi . Lazima utimize masharti yote hapa chini ili uweze kustahili:

  1. Wewe ni mpangaji Oregon na umechelewa malipo yako.

  2. Mmoja au zaidi ya wananyumba wako wanaweza kuonyesha jinsi janga la COVID-19 limeathiri moja kwa moja au kwa namna nyengine uwezo wa kulipa kodi au bili za matumizi.

  3. Mapato ya kila mwaka ya wanyumba wako ni ya au chini ya 80% ya Mapato Wastani ya Eneo ( Area Median Income) ya idadi ya watu nyumbani kwako. Tumia maelezo hapo chini ili ufahamu usatahili wako wa mapato.

Idadi ya watu nyumbani

Mapato wastani ya eneo ya 80% au chini

1 $54,150
2 $61,900
3 $69,650
4 $77,350
5 $83,550
6 $89,750
7 $95,950
8 $102,150

Maelezo kuhusu ulinzi dhidi ya kufukuzwa

Mswada wa 891 wa Bunge la Oregon unawalinda wapangaji ambao waliwasilisha maombi ya msaada wa kulipa kodi wasifukuzwe nyumbani kutokana na kutolipa kodi ikiwa watawasilisha hati za maombi yako kwa wamiliki nyumba.

Mpango wa Usaidizi wa Ukodishaji wa Dharura wa Jimbo la Oregon ulifungwa kwa waombaji wapya Jumatatu, Machi 21. Wapangaji wa Oregon waliotuma maombi ya msaada wa kulipa kodi kabla ya mpango huu kufungwa, na kumpa mwenye nyumba hati kabla ya tarehe 1 Julai 2022, wanalindwa na ulinzi huu wa "mpango wa usalama" hadi ombi lao lishughulikiwe, kufikia tarehe 30 Septemba, 2022. Ulinzi huu pia unatumika kwa wapangaji ambao tayari wamewasilisha hati kwa wamiliki wa nyumba zao na muda wa ulinzi wao wa awali uliisha walipokuwa wakisubiri msaada wao kufika.

Wapangaji wanaweza kupokea hati zinazostahili kutoka kwa  mhudumu wa msaada wa kulipa kodi anayewatumikia.

Ikiwa una maswali zaidi kuhusu vipi na lini unapaswa kuwasilisha thibitisho la maombi yako, tafadhali wasiliana na mhudumu wako wa msaada wa kulipa kodi au Kituo cha Sheria cha Oregon, Muungano wa Jamii wa Wapangaji au Huduma za Msaada wa Kisheria Oregon.

Tafadhali fahamu kuwa ulinzi mwingine wa wapangaji unaweza pia kupatikana kulingana na hali yako binafsi.

Jinsi ya kutimiza masharti ya kupokea ulinzi dhidi ya kufukuzwa nyumba

Wapangaji wanaweza kupokea hati zinazohitajika kutoka kwa  mhudumu wa msaada wa kulipa kodi anayewatumikia. Hati hizo lazima ziwasilishwe kwa mwenye nyumba kabla ya tarehe 1 Julai 2022, ili ulinzi dhidi ya kufukuzwa uanze kutekelezwa.

Ikiwa una maswali zaidi kuhusu vipi na lini unapaswa kuwasilisha thibitisho la maombi yako, tafadhali wasiliana na mhudumu wako wa msaada wa kulipa kodi au Kituo cha Sheria cha Oregon, Muungano wa Jamii wa Wapangaji au Huduma za Msaada wa Kisheria Oregon.