Kiswahili Rasilimali za Kupiga Kura na Chaguzi / Swahili Language Voting and Elections Resources 

Chaguzi za Kaunti ya Multnomah

Ukweli unaopaswa Kujua kuhusu Kupiga Kura na Chaguzi

Je, ni nani anayeweza kujisajili kupiga kura Oregon?

Unaweza kujisajili kupiga kura ikiwa unaishi (wewe ni mkazi wa) Oregon, wewe ni raia wa Marekanina una angalau miaka 16. Utapata kura yako ya kwanza kwa barua ukiwa na angalau miaka 18.

Unaweza kujisajili kupiga kura ikiwa una jinai kwenye rekodi yako na umekamilisha kutumikia kifungo chako. Pia unaweza kujisajili kupiga kura ikiwa huna makao au unakabiliwa na ukosefu wa nyumba. Unaweza kujisajili kupiga kura ikiwa huna anwani ya barua au makazi ya kudumu. Wasiliana na Chaguzi za Kaunti ya Multnomah kwa maswali kuhusu ustahiki wako wa kujisajili kupiga kura.

Je, ninajisajili vipi kupiga kura?

 • Jisajili kupiga kura mtandaoni kwenye tovuti ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Oregon oregonvotes.gov/register. Lazima uwe na leseni ya dereva au kitambulisho cha Oregon kujisajili mtandaoni.
 • Jisajili kupiga kura kwa kujaza karatasi Kadi ya Usajili wa Wapiga Kura ya Oregon. Unaweza kupata kadi ya karatasi kwenye ofisi ya Chaguzi za Kaunti ya Multnomah, maktaba yako ya umma, ofisi ya Idara ya Magari ya Oregon (Department of Moto Vehicles, DMV), au posta.
 • Ukitembelea Oregon DMV na upate leseni mpya ya dereva, kibali cha kuendesha gari, au kitambulisho unaweza kujisajiliwa kupiga kura bila kufanya chochote zaidi (mbinu ya Usajili Otomatiki wa Wapiga Kura wa Magari wa Oregon). Unaweza kusajiliwa kupiga kura kiotomatiki lakini haitatendeka wakati huo.

Wasiliana na Chaguzi za Kaunti ya Multnomah kwa maswali au usaidizi wa kujisajili kupiga kura.

Je, kupiga kura kwa njia ya barua kunafanyika vipi?

Chaguzi zote Oregon zinafanywa kulingana na ofisi ya chaguzi za kaunti. Ofisi ya chaguzi za kaunti inatuma kura kwa wapiga kura moja kwa moja. Wapiga kura wanajaza kura zao na kisha kuzirejesha kwenye ofisi ya chaguzi za kaunti kwa njia ya barua au kwenye Eneo Rasmi la Kuwasilisha Kura. Unaweza kupiga kura kwa njia ya barua Oregon kwa hatua sita rahisi:

 1. Jisajili kupiga kura mtandaoni, kwenye karatasi, au kupitia mbinu ya usajili otomatiki. Utapata Kadi ya Arifa ya Mpiga Kura katika barua. Kadi inathibitisha kuwa umesajiliwa kupiga kura. Pia unaweza kupiga simu au kutembelea Chaguzi za Kaunti ya Multnomah ili kupata maelezo.
 2. Wiki nne kabla ya uchaguzi utapata Kabrasha la Wapiga Kura katika barua. Kabrasha la Wapiga Kura ni kijitabu kilichoundwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oregon na Chaguzi za Kaunti ya Multnomah. Kabrasha la Wapiga Kura lina maelezo kuhusu wagombea na mabadiliko yanayopendekezwa kwenye sheria. Hawa wanaweza kuwa wagombea au zinaweza kuwa sheria za ndani (jiji, kaunti na wilaya), kwenye ngazi ya jimbo au taifa (nchi). Kabrasha la Wapiga Kura linapatikana mtandaoni kwenye oregonvotes.gov.
 3. Wiki mbili kabla ya uchaguzi utapata kura yako katika barua. Usipopata kura yako, wasiliana na Chaguzi za Kaunti ya Multnomah ili upate kura mpya.
 4. Piga kura kwa kujaza kura yako. Unaweza kuomba usaidizi kwa kutia alama kura yako au kuelewa jinsi upigaji kura unavyofanya kazi. Pindi unapoamua jinsi ya kupiga kura, tumia kalamu ya samawati au nyeusi kutia alama machaguo yako. Pia unaweza kuacha kitu bila kujaza. Unaweza kuandika mgombea wa shindano lolote. Ukikosea au ukipoteza kura yako, wasiliana na Chaguzi za Kaunti ya Multnomah ili upate kura mpya.
 5. Weka kura yako katika bahasha ya kurejesha kura ambayo haijalipiwa stempu. Lazima utie sahihi bahasha ya kurejesha kura ili kura yake ihesabiwe. Ikiwa utashinda kutia sahihi bahasha yako ya kurejesha kura kwa sababu ya ulemavu, wasiliana na Chaguzi za Kaunti ya Multnomah kwa usaidizi.
 6. Rejesha kura yako. Unaweza kutuma kura yako ukitumia bahasha ya kurejesha kura iliyolipiwa stempu (hakuna stempu inayohitajika) au unaweza kupeleka kura yako kwenye Eneo Rasmi la Kuwasilisha Kura. Kuna Maeneo Rasmi ya Kuwasilisha Kura ya saa 24 kwenye kaunti nzima, ikiwemo kila eneo la Maktaba ya Kaunti ya Multnomah. Unaweza kurejesha kura yako kwa barua au kwenye Eneo Rasmi la Kuwasilisha Kura. Ukirejesha kura yako kwa njia ya barua lazima itiwe alama ya posta mnamo au kabla ya Siku ya Uchaguzi. Kura zinazorejeshwa kwenye Eneo Rasmi la Kuwasilisha Kura lazima zirejeshwe kufikia saa 8:00 usiku Siku ya Uchaguzi.

Je, ninaweza kupata usaidizi wa kupiga kura kwa lugha ninayoipenda?

Ndiyo. Chaguzi za Kaunti ya Multnomah inatoa mkalimani bila malipo kwa yeyote anayehitaji usaidizi wa hatua yoyote ya kupiga kura ikiwemo:

 • Kujisajili kupiga kura
 • Kutia alama au kusoma kura
 • Kusasisha anwani, jina, chama cha siasa au maelezo mengine ya mpiga kura
 • Kuelewa sheria na hatua za chaguzi za kupiga kura
 • Usaidizi unaohusiana na uchaguzi mwingine wowote.

Usaidizi huu huwa wa bila malipo. Kwa usaidizi, piga simu, tuma barua pepe au tembelea ofisi ya chaguzi. Ukalimani wa simu unapatikana kwa lugha yoyote na kuna wafanyakazi wa uchaguzi wanaozungumza lugha mbili (Kihispania). Pia unaweza kuwasiliana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oregon, Kitengo cha Chaguzi ili kuomba mkalimani.

Je, ninaweza kupata usaidizi wa kupiga kura ikiwa nina ulemavu?

Ndiyo. Chaguzi za Kaunti ya Multnomah inatoa usaidizi wa kupiga kura na unaohusiana na chaguzi kwa wapiga kura walio na ulemavu. Chaguzi za Kaunti ya Multnomah inaweza kukusaidia nyumbani kwako au kwenye ofisi ya chaguzi. Usaidizi huu huwa wa bila malipo. Piga simu, tuma barua pepe, au tembelea Chaguzi za Kaunti ya Multnomah kwa usaidizi katika hatua yoyote ya kupiga kura ikiwemo:

 • Kujisajili kupiga kura
 • Kutia alama au kusoma kura
 • Kusasisha anwani, jina, chama cha siasa au maelezo mengine ya mpiga kura
 • Kuelewa sheria na hatua za chaguzi za kupiga kura
 • Usaidizi unaohusiana na uchaguzi mwingine wowote.

Chaguzi za Kaunti ya Multnomah inataka uweze kupiga kura kwa urahisi, kwa faragha na kwa uhuru, kuelewa hatua za kupiga kura, kuelewa sheria za chaguzi na kujua mtu wa kumwomba usaidizi. Kila hali ya mpiga kura ni tofauti. Tafadhali wasiliana na Chaguzi za Kaunti ya Multnomah kwa usaidizi.

Anwani ya Chaguzi za Kaunti ya Multnomah:

1040 SE Morrison Street, Portland OR 97214

Simu: 503-988-8683 Barua Pepe: elections@multco.us

Tovuti: MultnomahVotes.gov

Je, nitamwuliza nani nikiwa na maswali zaidi?

Wasiliana na Chaguzi za Kaunti ya Multnomah:

Saa: Jumatatu - Ijumaa saa 8:00 asubuhi - saa 5:00 jioni. Piga simu kuhusu saa za ziada za ufunguzi karibu na uchaguzi.

Anwani: 1040 SE Morrison Street, Portland, OR 97214

Simu: 503-988-8683 | Faksi: 503-988-3719 | TTY Rilei: 1-800-735-2900

Barua pepe: elections@multco.us

Wasiliana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oregon, Kitengo cha Chaguzi:

Simu: 1-866-673-8683 | Faksi: 503-373-7414 | TTY Rilei: 1-800-735-2900

Barua pepe: elections.sos@state.or.us